24 Mei 2014 - 19:17
Mamia ya Wasomalia wafukuzwa nchini Kenya

Jumuiya haki za binadanu imetangaza kuwa: Serikali ya Kenya yawafukuza mamia ya wasomalia wanaoishi kikimbizi nchini humo, huku wakiwa katika mapambano na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab kinachofungamana na kikundi cha kigaidi cha Alqaida.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jumuiya ya haki za binadamu imeongeza kusema kuwa: viongozi wa Kenya katika maamuzi yake kukabilana na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab wameamua kuwakamata raiya wa Somalia na kuwarudisha nchini kwao.
Msimamizi wa haki za binadamu amesema kuwa: kulirudisha kundi la nne la wasomalia siku ya jumanne nchini kwao  kimekamilisha idadi ya wasomali hao kufikia 359, msimamizi huyo aliongeza kusema kuwa; kuwarudisha wasomalia hao makwao ambako ni maeneo yasiokuwa na amani nchini humo nikinyume na matakwa yao, kwakuwa nchini humo hali ya amani bado haijakuwa sawa na suala hilo nikuwafanyia kinyume na haki na kanuni.
Katika hali hiyo jumuiya ya kimataifa ya wakimbizi imeonyesha hofu yake katika suala hilo. Papo hapo  kikundi cha Al-shabaab siku ya alhamisi kimetishia kuamishia vita nchini Kenya, nakuwataka wapiganaji wa Al-shabaab kufanya mashambulio katika mji mkuu wa Nairobi.
Jeshi la Kenya mnamo mwaka 2011 liliingia kusini mwa Somalia kwaajili ya kupambana na magaidi wa Al-shabaab nabaadae kuungana na jeshi la umoja wa Afrika, ambapo suala linaafikiana na maamuzi ya jumuiya ya umoja wa mataifa katika kupambana na kikundi hicho cha kigaidi.
katika hali hiyo nchi za kimagharibi zimewatahadharisha wananchi wake kusafiri na kutembelea mikoa ya “Mwambasa” kutokana na vitisho hivyo.